Kocha mpya wa Yanga Hans              Pluijm leo amefanya mkutano wa kwanza na waandishi wa habari              tangu apewe mikoba ya kuifundisha tena timu hiyo yenye              maskani mitaa ya Kariakoo jijini Dar E s Salaam. Mkutano huo              umefanyika Jangwani, kifupi alichosema ni kwamba amefurahi              kurudi Yanga paia amesisitiza kuendeleza utamaduni wake wa              kufundisha soka la kuvutia ikiwa ni pamoja na kushambulia,              mambo ambayo yatawafanya wanayanga kuwa na furaha,amesema              amewaambia wachezaji wake kwamba hakuna mafanikio ya mtu              mmoja,iwapo watajituma na kuwapa ushirikiano benchi la              ufundi pamoja na viongozi basi mafanikio mengi yatakuja.
        Van Pruijm anasema anajua              kazi kubwa iliyopo mbele yake hasa mchezo ujao dhidi ya azam              na kesho wanaingia kambini kujiwinda na mchezo huo.
        
Comments
Post a Comment