Kinda mchawi wa soka kutoka Norway, Martin Odegaard anatarajiwa kuzitembelea Manchester United na Manchester City wiki ijayo katika kile kinachoonekana kama ni njia yake ya kuchagua timu ya kujiunga nayo.
Dogo huyo mwenye umri wa miaka 16 mwenye uwezo wa hali ya juu wa kutandaza soka, anataka kuzitembelea klabu zote kubwa zinazosaka saini yake.
Martin Odegaard anayecheza nafasi ya kiungo, tayari alishatembelea mazoezi ya Manchester United mapema msimu huu, lakini anataka kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
City ilishaanza kufanya maongezi na klabu ya kinda huyo, Stromsgodset lakini timu hiyo ya Norway imesema mchezaji huyo yuko huru kuamua wapi pa kwenda.
Bayern Munich inaamini wana nafasi nzuri ya kumsani kinda huyo, lakini inajua wazi kuwa Odegaard alifurahia maisha yake ya siku mbili ndani ya Liverpool, klabu anayoishabikia tangu utotoni mwake.
Comments
Post a Comment