MAONYESHO YA KWANZA YA KIMATAIFA YA VIPAJI MPIRA WA MIGUU KWA VIJANA WALIOKO SHULENI NA VYUONI, TANZANIA DESEMBA 19 – 21 2014


MAONYESHO YA KWANZA YA KIMATAIFA YA VIPAJI MPIRA WA MIGUU KWA VIJANA WALIOKO SHULENI NA VYUONI, TANZANIA DESEMBA 19 – 21 2014
Tunayo furaha kukujulisheni kuwa taasisi ya Boko Beach Veterans Sports Club (BBV) itaandaa maonyesho ya kimataifa ya vipaji vya mpira wa miguu kwa vijana wa mashuleni na vyuoni, kuanzia tarehe 19 had 21 kwenye uwanja wao wa kisasa ulioko maeneo ya Boko, Kinondoni , Dar es salaam.  

Maonyesho haya ni nafasi dhahiri kwa vijana wenye vipaji vya kusakata mpira wa miguu, wavulana kwa wasichana, kucheza soka nchini Marekani huku wakisoma katika vyuo vya nchini humo kwa kulipiwa gharama zote. Makocha wapatao watatu (3) kutoka katika chuo kikuu cha Alabama, Chuo kikuu cha Martin Methodist and chuo kikuu cha Lindsey Wilson wamesha thibitisha kushiriki na tunawategemea kufika tarehe 15 Desemba 2014.
 Maonyesho haya yanatilia mkazo kwa usawa kipaji na mpira wa miguu pamoja na uwezo wa kielimu. 
Pia yanawapa vijana wa kitanzania nafasi ya kupata udhamini wa kusoma katika vyuo vikuu vya Marekani. Ni mpango wa ufadhili ambao unawaunganisha vijana wa kitanzania wenye ndoto ya kucheza mpira pamoja na kusoma na ulimwengu mzima. Boko Beach Veterans Sports Club (BBV)  tayari tumekwisha alike shule mbali mbali kuleta washiriki.

Mkakati wa BBV to ni kuonyesha kile ambacho kimekuwa kikifanywa nan chi nyinngine katika kuinua ujuzi wa kucheza mpira wa miguu kwa vijana wao, kwa kuhakikisha kuwa michezo na elimu vinaenda sambamba. Wakiwa na elimu, wachezaji wa mpira wa miguu wanaweze kutengeneza maisha yao baada ya kustaafu kucheza, kwa kuajiriwa, kuanzisha shughuli zao au kuwa makocha wazuri. 
Pamoja na kuwa na wachezaji wengi walio

wahi kuwika Tanzania, ni wacheche sana wameweza kuwa na maisha mazuri baada ya kustaafu kucheza, sababu kubwa ikiwa ukosefu wa elimu bora. 

BBV inakukaribisha sana kushiriki katika maonyesho haya ya kwanza nay a aina yake na yenye mweleleo wa kuleta faida kubwa binafsi kwa washiriki na kwa taifa kwa ujumla. BBV ina nia ya kuandaa maonyesho haya kila mwaka ikiwa ni mchango wake katika kampeini za TFF na serikali ya kuinua kiwango cha soka nchini. 


Comments