BAO la Radamel Falcao dakika ya 52
limeunusuru Manchester United kulala mbele ya Aston Villa baada ya kulazimisha sare ya 1-1 Uwanja wa Villa Park jioni ya leo.
Villa ilimaliza pungufu mechi hiyo baada ya mchezaji wake, Gabriel Agbonlahor kutolewa kwa kadi nyekundu katikati ya kipindi cha pili baada ya kumchezea rafu Ashley Young.
Lakini iliweza kupata bao la kuongoza dakika ya 18 kupitia kwa Christian Benteke aliyefumua shuti kwa mguu wa kushoto, kabla ya Falcao kuunganishwa kwa kichwa krosi ya Ashley Young kuisawazishia United.
Kikosi cha Aston Villa kilikuwa; Guzan, Okore, Vlaar, Clark, Lowton, Sanchez, Delph, Weimann/
N'Zogbia dk80, Cissokho/Bacuna dk80, Benteke na Agbonlahor
Man Utd; De Gea, Jones, Carrick, Evans,
Valencia/Wilson dk74, Fletcher/Fletcher dk46, Rooney, Mata, Young, Van Persie/Di Maria dk62 na Falcao.
Comments
Post a Comment