wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Bromwich Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa The Hawthorns.
Mabao ya City leo yamefungwa na Fernando dakika ya nane, Yaya Toure kwa penalti dakika nane baadaye na David Silva dakika ya 34.
City inafikisha pointi 42 kwa ushindi huo na kuendelea kubaki nafasi ya pili, nyuma ya vinara Chelsea wenye pointi 45, baada ya timuBzote kucheza mechi 18. Bao pekee la WBA limefungwa na Ideye dakika ya 86.
Kikosi cha West Brom kilikuwa; Foster,
Wisdom, McAuley, Lescott, Pocognoli/Gamboa dk67, Morrison, Mulumbu, Sessegnon, Gardner/ Brunt dk67, Varela/Ideye dk67 na Berahino.
Manchester City: Hart, Sagna, Demichelis, Mangala, Clichy, Fernando, Toure/Fernandinho dk69, Jesus Navas, Silva/Kolarov dk63, Nasri/ Lampard dk75 na Milner.
Comments
Post a Comment