MAN CITY NAYO HOI YABANWA NA KULAZIMISHWA SARE 2-2 NA BURNLEY NYUMBANI


MAN CITY NAYO HOI YABANWA NA KULAZIMISHWA SARE 2-2 NA BURNLEY NYUMBANI
 MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Burnley usiku huu
Uwanja wa Etihad.

David Silva alianza kuwafungia City dakika ya 23 kwa shuti la umbali wa mita 18 akimtungua kipa wa Burnley, Tom Heaton kabla ya Fernandinho kufunga la pili dakika ya 33.

Burnley ikazinduka na kusawazisha mabao yote hayo kupitia kwa George Boyd dakika ya 47 na Ashley Barnes dakika ya 81.
 Kikosi cha Man City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Demichelis, Mangala, Kolarov, Fernando, Fernandinho/Sinclair dk88, Jesus Navas, Silva, Nasri/Lampard dk76 na Milner/Jovetic dk62.

Burnley: Heaton, Trippier, Keane, Shackell, Mee, Boyd, Marney, Jones, Arfield, Ings na Barnes.


Comments