LIVERPOOL YAIFANYIA MAUAJI SWANSEA, YAICHAPA 4-1 … Gerrard asugua benchi, Lallana Man of the Macth


LIVERPOOL YAIFANYIA MAUAJI SWANSEA, YAICHAPA 4-1 … Gerrard asugua benchi, Lallana Man of the Macth

Three Swansea players look on as Lallana sends a              left-footed finish past Fabianski to send Liverpool into a              commanding lead

Upepo mbaya unaanza kumwepuka kocha wa Liverpool Brendan Rodgers baada ya timu yake kufanya kweli kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Swansea.

Liverpool ikaingushia kipigo cha 4-1 Swansea, huu ukiwa ndio ushindi wao mkubwa zaidi msimu huu, shukran za dhati zimwendee kiungo Adam Lallana aliyeng'ara vilivyo na kutupia wavuni mipira miwili.

The former Southampton midfielder faces the Kop in              celebration of his second goal of the night against Swansea

Kiungo huyo wa zamani wa Southampton alifunga katika dakika ya 51 na 61 hii ikiwa ni baada ya Moreno kuifungia Liverpool bao la kwanza dakika ya 33.

Lallana stands waiting for his team-mates to join him              after giving Liverpool a 3-1 lead on Monday night

Swansea walipata bao la pekee katika dakika ya 52 kupitia kwa Sigurdsson, lakini beki wake Jonjo Shelvey akajifunga dakika 68 na kuhitimisha karamu ya Liverpool.

Katika hali inayoonyesha dalili za kutemwa taratibu, Steven Gerrard akasugulishwa benchi mwanzo mwisho, huku Brendan Rodgers akifurahia namna timu yake ilivyodhibiti eneo la kiungo bila nahodha wake huyo.

Liverpool (3-4-2-1): Mignolet 7; Can 7, Skrtel 7, Sakho 6; Manquillo 6, Henderson 8, Lucas 7, Moreno 8; Lallana 8 (Markovic 77 6), Coutinho 8 (Borini 89'); Sterling 6 (Balotelli 82').

Swansea (4-2-3-1): Fabianski 5; Richards 5 (Rangel 46 5), Fernandez 6, Williams 6, Taylor 5; Britton 6 (Ki 66'), Shelvey 4; Dyer 5.



Comments