BAO pekee la Raheem Sterling limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Burnley Uwanja wa Turf Moor katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.
Mshambuliaji hiyo kinda wa miaka 20 wa kimataifa wa England, alifunga bao zuri baada ya kumzunguka kipa Tom Heaton.
kabla ya kuusukumia mpira nyavuni.
Huo ni ushindi wa kwanza kwa Liverpool katika Ligi Kuu ya England msimu huu tangu walipoifunga 3-1 Leicester City Desemba 6, mwaka huu.
Comments
Post a Comment