Kocha wa Newcastle Alan Pardew sasa ni kocha mpya wa Crystal Palace baada ya vilabu hivyo viwili kukubaliana fidia ya pauni milioni 2.
Alan Pardew aliweka wazi kuwa anataka kutimka Newcastle na kwenda kujiunga na timu aliyoichezea enzi zake za kutandaza soka ambapo tajiri yake Mike Ashley hakuwa na pingamizi na akadai fidia ya pauni milioni 2 badala ya pauni milioni 5 iliyostahili.
Kocha huyo ambaye mara kadhaa amekuwa akikutana na mabango ya mashabiki wa Newcastle yalotaka atimuliwe, atasaini mkataba wa miaka minne Crystal Palace, dili lenye thamani ya pauni milioni 2 kwa mwaka.
Katika enzi zake za uchezaji, Pardew aliichezea Palace mechi 128 kati ya mwaka 1987 na 1991 na kuifungia mabao manane.
Comments
Post a Comment