Imekuwa ni vigumu kwa msimu huu, kumfunika kipa wa Manchester United David De Gea, lakini Jumapili hii mlinda mlango wa Tottenham Hugo Lloris amefanya hivyo baada ya kuwa shujaa wa kupangua mashuti ya washambuliaji wa United.
Katika dakika ya 45 za mwanzo Hugo Lloris akapangua michomo ya kadhaa ya Falcao na Robin van Persie ambayo ni wazi kuwa bila umahiri wake, basi Tottenham ingekwenda mapumziko ikiwa imeshabugizwa zaidi ya mabao mawili.
Dakika ya 34 Lloris alifanya kazi ya ziada kuodoa hatari iliyosukumizwa na Falcao, kabla nafasi nzuri zaidi ya kipindi hicho cha kwanza haijamdondokea Van Persie.
Michael Carrick alimtengea mpira mzuri Van Persie, akiwa amebaki yeye na Lloris ndani ya kisanduku cha sita, badala ya kufunga akaamua kuremba, Lloris akamdhibiti kwa mguu wake mithili ya sentahafu.
Muda mfupi baadae Lloris akacheza vizuri krosi ya Ashley Young, kabla ya kupangua mkajwa wa Juan Mata.
Kipindi cha pili kilikuwa cha mashambulizi ya kupokezana ingawa ni Tottenham iliyokuwa nyumbani ndiyo iliyokuwa hatari zaidi lakini hadi mwisho wa mchezo si United wala Tottenham iliyopata bao.
Tottenham: Lloris 8, Chiriches 6, Fazio 6, Vertonghen 6, Davies 6, Stambouli 5.5, Mason 5.5, Townsend 6 (Dembele 79 mins), Eriksen 5.5, Chadli 5 (Lamela 79), Kane 6.
Manchester Utd: De Gea 6, Jones 6.5, McNair 5 (Shaw 75), Evans 6 (Smalling 72), Carrick 7.5, Valencia 5.5 (Rafael 46), Mata 7.5, Rooney 6.5, Young 7, van Persie 5, Falcao 4.
Comments
Post a Comment