Katibu mkuu mpya wa Yanga atangaza mikakati yake ya kuhakikisha Klabu inajiendesha kiuchumi



Katibu mkuu mpya wa Yanga atangaza mikakati yake ya kuhakikisha Klabu inajiendesha kiuchumi
Katibu mpya wa Yanga Dk. Jonas Tiboroha, ametangaza mikakati yake ya kuhakikisha Yanga inajiendesha kiuchumi ikiwa ni pamoja na kupitia upya mikataba yote ya wadhamini.

Akizungumza Makao Makuu ya Klabu hiyo leo, Tiboraha alisema kuwa Yanga ni klabu kubwa hiyo ni wakati wa kujiendesha yenyewe badala ya kutegemea mtu binafsi na kwamba haiwezi kuwa na mikataba ambayo haikithi maslahi ya klabu hiyo.

"Yanga ni bidhaa inayojiunza yenyewe uwezi kuingia mkataba wake sawa na Stand United, haiwezekani ikapata mgao sawa kama wanafunzi wa shule ya msingi unawapanga mstari unawambia haya kila mtu unamgawia pipi moja moja na wanaridhika, haiwezekani ni lazima Yanga iwe tofauti.

"Klabu kama Liverpol, inawashabiki wengi hata kama haipo kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi linapokuja suala la mgao wa fedha inapata fungu kubwa kwa vile tayar inajiuza, sasa Yanga ingie mikataba sawa na kina Stand United dunia nzima itatushangaa."alisema.

Alisema sekreatrieti mpya ambayo wanaiongoza ipo kwenye mchakato wa kupitia upya mikataba ya TBL, Vodacom na Azam ambayo hadi sasa klabu hiyo ya Jangwani imesusia fedha zake wakidai nyongeza kwa vile hawawezi pata mgao sawa na timu nyingine. 

Hata hivyo Tiboraha ambaye ni mwana Falsafa wa Michezo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema mpira wa Tanzania umegubikwa na changamoto kubwa na kwamba miezi minne aliyofanya kazi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), amegundua Yanga kuna mambo mengi ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili iweze kutoka hapo ilipo na kusonga mbele.

"Katika maisha yangu ya mpira dunia, hakuna timu inayoendelea bila kujenga uwzo binafsi, lazima tujenge uwezo wa timu kujiendesha yenyewe kimaslahi, kuwekeza kwa vijana wadogo nitahakikisha nalisimamia hilo.

"Klabu za Tanzania sio Yanga tu, zimekuwa na utamaduni wa kukimbilia kusajili wachezaji kwa mamilioni, garama kubwa wakati wangewekeza kwa vijana hata timu ya Taifa ingekuwa bora na tungefanya vizuri kwenye michuano mbali mbali ya kimataifa.

"Mfano Msuva (Simon) nilimfundisha mimi, mazoezi alikuwa akifanyia pale UDSM, niliwambia Yanga mchukueni huyu kijana, wakadengua akachukuliwa na timu nyingine matokeo yake Yanga wamekuja kumsajili kwa gharama kubwa."

"Ligi ya Tanzania ni dhaifu, nikikumbuka wakati mdogo klabu kama yanga ilikuwa na timu A mpaka C, wachezaji wanakuzwa na ndio waliowika siku za nyuma lakini sasa hivi tunakimbilia kusajili wachezaji wa nje kwa garama kubwa, wengine ndio unakuta klabu zinaingizwa mkenge kwa kusajili wachezaji bomu kwa vile hawawajui.

"Mabadiliko natakas yaanzie Yanga, klabu zikijenga utaratibu huu hata Ligi itakuwa imara na hazitakimbilia kusajili wachezaji wa nje, chukulia mfano Azam ina kila kitu lakini ukiangalia 'quality' walionao hawaendani na uwekezaji uliofanywa.

"Kwa hapa nchi tunasema Azam klabu bora kwa vile msimu uliopita imecheza mechi zote bila kufungwa, lakini hiyo haitoshi kusema ni bora, utasema bora kama italeta ushindani kwenye michuano ya kimataifa sio inacheza raundi ya kwanza ya pili inatolewa, uwezi ifunga Stand United bao tatu ukajisifu wewe bora, kama unaweza kuifunga tatu, ikicheza na Esparance, TP Mazembe au Motemapembe itafungwa 18,  kwa sababu 'quality' ya wachezaji Tanzania bado sana, tunataka Yanga ianze kuwa mfano.

Katika hatua nyingine, Tiboraha alisema kuwa hana wasiwasi na kutimuliwa Yanga iwapo uwezo wake utaonekana mdogo kutoka na historia ya klabu hiyo ambayo ndani ya miaka miwili chini ya mwenyekiti Yusuf Manji wameshafungashiwa virago makatibu watatu akiwemo Laurance Mwalusako, Selestine Mwesigwa ambaye ameuburuza uongozi huo mahakamani pamoja na Benno Njovu ambaye nafasi yake imechukuliwa na Tiboraha.

"Nimejiandaa kwa lolote ninachofahamu wengine mikataba yao imeisha ndio maana wameondoka wengine hawajaperfome, hata mimi kama sina onyesha uwezo nipo tayari kuwajibika."


Comments