JEMEDARI SAID; ‘KAMBI YA KAMPALA ITATUIMSARISHA ZAIDI KWA LIGI KUU NA KLABU BINGWA AFRIKA’


JEMEDARI SAID; 'KAMBI YA KAMPALA ITATUIMSARISHA ZAIDI KWA LIGI KUU NA KLABU BINGWA AFRIKA'

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,

Kabla ya kuanza kwa msimu uliopita wa ligi kuu ya Tanzania Bara, 2013/14 klabu ya Azam FC ilifanya ziara ya maandalizi nchini Afrika Kusini na huko waliweka kambi ya wiki moja na siku kadhaa na hakika iliwasaidia kwani ni msimu ambao walitwaa ubingwa wa kwanza wa ligi kuu.
JEME
Kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya msimu huu, Azam ilikuwa katika michuano ya riki na klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup nchini Rwanda na huko ilifanikiwa kucheza michezo mitano hadi ilipondolewa na El Merreikh ya Sudan Kasskazini kwa changamoto ya mikwaju ya penalti katika hatua ya robo fainali.

Michezo hiyo ya Kagame iliweza kukiimarisha kikosi hicho ambacho kilikuwa na machaguo kadhaa mapya. Didier Kavumbagu, Leonel Saint na Ismael Diarra walikuwa wachezaji wapya wa kigeni ambao waliungana na Shomari Kapombe kutengeneza idadi ya wachezaji wapya. Msimu ulipoanza timu hiyo ilifanikiwa kushinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Polisi Morogoro lakini katika michezo saba tayari wamepoteza mara mbili dhidi ya JKT Ruvu ( katika uwanja wa Chamanzi) na Ndanda FC.

Chini ya Joseph Omog timu hiyo imewaongeza wachezaji wawili wa kigeni na kuwatema Saint na Diarra. Kiungo mshambulizi, Amri Kiemba ametua kwa mkopo akitokea Simba SC, huku mshambulizi aliyefanya vizuri katika Kagame Cup akiwa na KCCA, Mganda, Brian Majwega akiungana na mlinzi bora wa michuano hiyo, Muivory Coast, Pachal Serge Wawa aliyekuwa akiichezea Merreikh waliotwaa ubingwa ili kujiimarisha na michuano ya ndani na ile ya klabu bingwa Afrika ambayo watashiriki kwa mara ya kwanza mapema mwaka ujao.

Timu hiyo imeweka kambi ya muda nchini Rwanda kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Yanga SC siku ya Jumapili ya wiki ijayo. Azam tayari imecheza na URA na SC Villa na inataraji kucheza michezo mingine miwili kabla kurudi nyumbani siku ya Jumatatu ijayo. Akizungumza na mtandao huu akiwa Kampala, Uganda, Meneja wa timu hiyo, Jemedari Said Kazumari amesema kuwa wameweza kujifunza mengi kutoka kwa wenyeji wao na kudai kuwa kambi hiyo inawasaidia kwa kiasi kikubwa.

" Hakuna tofauti kubwa sana na ilivyokua South Africa, unapocheza na timu ambazo unadhani aidha umezizidi au uko nazo sawa halafu matokeo yakawa hasi kwako unapata kujifunza kujua lilipo tatizo. Watanzia wengi tunaamini kwamba ligi yetu ni bora East Africa na ina ushindani kuliko zingine ukipigwa unajiangalia mara mbili mbili, na uzuri ni kwamba baada ya vipigo viwili kila mtu imeshtua "

" Kumbuka huko Champions league timu ni imara kuliko hizi. Ingawa matokeo kwenye mechi kama hizi huyapi umuhimu sana kwani ni ' test matches' tu za kukuonyesha udhaifu, lakini yanakupa mwanga wa kiasi gani uko dhaifu au imara. Timu kama URA inatumia nguvu na kasi sana kiwanjani na right from the start wanakushambulia. Aina ya mchezo ambao Tanzania kupata ni nadra. "

" Villa wakitumia flanks karibu muda wote na walifanikiwa kila mara kufika uongozi wetu wa magoli na hatimaye kutufunga 3-2. Hilo ni somo na linafanyiwa kazi namna gani tuliruhusu magoli 2 ktk dakika 3! Tumepata umoja na utulivu kama ambao tulipata Johannesburg."



Comments