Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Azam FC wamepangwa kucheza dhidi ya El Merrikh ya Sudan katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika mwakani huku Yanga SC wakipewa timu ya BDF XI ya Botswana katika michuano ya Kombe la Shirikisho mwakani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye mtandao rasmi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) leo, droo ya michuano ya 19 ya Klabu Bingwa Afrika mwakani na michuano ya 12 ya Kombe la Shirikisho barani imechezeshwa kwenye makao makuu ya CAF jijini Cairo, Misri leo asubuhi, klabu 58 zikichuana katika Klabu Bingwa na 56 katika Kombe la Shirikisho.
Faida ya Azam FC na Yanga SC katika michuano hiyo mwakani ni kwamba zitaanzia nyumbani Februari kabla ya kwenda ugenini Machi.
MITIHANI
Mshindi wa mechi baina ya Yanga SC na BDF XI FC atakutana na
mshindi kati ya Sofapaka FC (Kenya) dhidi ya Platnum FC ya Ligi Kuu ya Zimbabwe katika hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho, wakati mshindi kati ya Azam FC na El Merrikh FC ya iliyotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Sudan mara 19 tangu ianzishwe 1927, atachuana na mshindi kati ya Lydia Ludic B.A (Burundi) dhidi ya Kabuscorp do Palanca FC ya Angola katika hatua ya kwanza ya Klabu Bingwa ya Afrika.
Yanga ilitolewa kwa matuta mwaka huu na Al Ahly katika hatua ya kwanza ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya timu zote kufunga bao 1-0 katika mechi zote mbili. Kila imu ilishinda nyumbani.
Kabla ya kuivaa Yanga SC ilitoa kwa idadi kubwa ya mabao Timu ya Komorozine ya Visiwa Comoro katika hatua ya awali ya michuano hiyo maka huu.
Azam FC ilitolewa hatua ya awali na klabu ya Ferroviario ya Msumbiji.
Comments
Post a Comment