TAARIFA za uhakika kutoka Simba zinaeleza kuwa kocha mpya anayekuja kurithi mikoba ya Mzambia Patrick Phiri, Mserbia Goran Kapunovic anatua kesho majira ya saa 1:00 asubuhi katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Kocha huyo anatarajia kusaini mkataba wa kuifundisha Simba na ataanzia katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayoanza Januari Mosi mpaka 13 mwakani.
Goran atasaidiwa na Mnyarwanda Jean Marie Ntagwabira anayechukua nafasi ya Seleman Matola anayetupwa Simba B.
Wakati huo huo, Kocha Phiri aliiongoza Simba katika mazoezi leo na alipoulizwa kuhusu kuachishwa kazi yake alisema yeye hajui kitu, anachokijua ni kwamba yupo ndani ya Simba.
"Bado nipo ndani ya Simba, naiandaa timu yangu na kesho tunaondoka kwenda Zanzibar". Alisema Phiri.
Comments
Post a Comment