Likiwa na albam yao mpya mkononi "Kichambo Kinakuhusu" kundi zima la Five Stars litajitosa Lugoba ndani ya ukumbi wa Lugoba Carnival na kufanya onyesho maalum la mkesha wa mwaka mpya.
Mkurugenzi wa kundi hilo, Ally Jay ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo litafanyika Jumatano usiku ambapo watawapa wakazi wa Lugoba na maeneo ya jirani uhondo wa nyimbo mpya pamoja na zile za zamani.
Comments
Post a Comment