Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas
NYOTA wa Chelsea, Cesc Fabregas ameachwa katika kikosi bora cha msimu huu kilichochaguliwa na Gary Neville na Jamie Carragher na badala yake ameingizwa kiungo wa Southampton, Morgan Schneiderlin.
Carragher alitaka kumuweka Fabgregas katika kikosi chake kutokana na kupiga pasi za mwisho 13 msimu huu, lakini Veville alimchagua Schneiderlin.
Kura ziliamuriwa na watazamaji wa Sky Sports kupitia mtandao wa kijamii wa Twita ambapo kiungo huyo wa 'Watakatifu' amemshinda Fabregas.
Schneiderlin alipata asilimia 62 ya kura zote.
Hii ndio timu muunganiko iliyochaguliwa na Gary Neville na Jamie Carragher
Comments
Post a Comment