KOCHA WA BRAZIL, DUNGA HAJATAKA KUFICHA SAAANAA MAMBO, AMEWEKA WAZI KABISA KWAMBA KURA YAKE YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA MAARUFU KAMA BALLON D'OR AMEMPIGIA MSHAMBULIAJI WA REAL MADRID, CRISTIANO RONALDO.
DUNGA AMESEMA HAYO WAKATI WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI NCHINI BRAZIL. WENGINE WANAOWANIA TUZO HIYO NI MSHAMBULIAJI WA ARGENTINA, LIONEL MESSI NA KIPA WA BAYERN MUNICH, MANUEL NEUR.
MSHINDI ANATARAJIA KUTANGAZWA JANUARI 12, MWAKANI. LAKINI ZOEZI LA UPIGAJI KURA KWA MAKOCHA NA MANANODHA LINAELEZWA KUKAMILIKA.
Comments
Post a Comment