DROGBA ASEMA HASHANGAZWI NA KASI YA MANCHESTER CITY …akiri ligi ni mchuano ni mgumu


DROGBA ASEMA HASHANGAZWI NA KASI YA MANCHESTER CITY …akiri ligi ni mchuano ni mgumu

Mshambuliaji mkongwe wa Chelsea Didier Drogba amesema hashangazwi na kasi ya upinzani wa kupigania taji kati ya timu yake na Manchester City na kwamba ni jambo alililolitegmea.

Chelsea ilianza ligi kwa kishindo na kuwa mbele kwa pointi 8 dhidi ya Manchester City lakini sasa hivi ni pointi tatu ndizo zinawatenganisha na ingeweza kuwa pointi moja tu kama vijana wa Manuel Pellegrini wasingefanya uzembe na kuruhusu sare ya 2-2 kwa Burnley.

Drogba anasema hashangazwi kupungua kwa wigo wa pointi. "Nadhani itakuwa ni ligi ngumu," alisema. "Tulijua wazi kuwa ligi haijaisha.

"Miaka michache iliyopita, nadhani tulikuwa mbele ya Manchester United kwa pointi 11 au 12, lakini mwisho wa siku wao wakawa mabingwa.

"Hivyo pointi nane au tisa – sijui ni pointi ngapi tuko mbele ya Manchster City – lakini nadhani haitoshi.

"Katika msimu huo ilikuwa ni mapema sana, lakini nadhani sasa tumeanza vizuri tena, mapambano yanaendelea."

Chelsea itaingia mwaka 2015 ikiwa kileleni mwa ligi na ilikuwa hivyo pia kipindi cha Christmas.

Jose Mourinho hajawahi kuachia taji limponyoke katika kipindi chote ambacho timu yake imekuwa ikiongoza ligi wakati wa Christmas - ameshinda mara saba katika hali hiyo kwenye ligi mbali mbali.



Comments