COASTAL UNION YATAMBA KUIUA PRISONS MBEYA


COASTAL UNION YATAMBA KUIUA PRISONS MBEYA

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Mabingwa wa 1988 wa Tanzania Bara, Coastal Union ya Tanga, wamerejea jijini humo baada ya kuichapa mabao 3-1 timu ya Combine ya Mombasa jijini Mombasa, Kenya jana.
cos
Aidha, Wagosi hao wa Kaya wametamba kuwa kikosi chao kimeimarika na sasa kiko tayari kwa ajili ya kutembeza virungu kwenye kambi ya Magereza jijini Mbeya kitakapoivaa timu ya maafande wa Tanzania Prisons katika mechi yao ya raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) itakayochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya mwishoni mwa wiki.

Msemaji wa Coastal Union Oscar Assenga amesema kikosi chao kimerejea salama jijini Tanga leo kikitokea Mombasa kilikoshinda mabao 3-1 dhidi ya wenyeji wao. Shukrani kwa mabao ya Rama Salim aliyefunga mawili na Itubu Imbem yaliyompa ushindi wa kwanza kocha mpya wa Coastal Mkenya James Nandwa.

"Sasa tuko tayari kwa mwendelezo wa Ligi Kuu, tutaanza na Prisons. Ndani ya siku tatu tutakuwa tumeshaanza safari ya kwenda Mbeya kuwavaa maafande hao wa Magereza," amesema Assenga.



Comments