TIMU ya Chelsea leo imeshinda mechi ya tatu mfululizo ya Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa West Ham United mabao 2-0 Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Beki na Nahodha, John Terry aliifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 31 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Diego Costa.
Diego Costa mwenyewe akafunga bao la pili dakika ya 62 akimalizia pasi ya Eden Hazard, kabla ya kumpisha mkongwe Didier Drogba dakika ya 83.
Comments
Post a Comment