CHELSEA YAICHAPA STOKE CITY 2-0 LIGI KUU ENGLAND


CHELSEA YAICHAPA STOKE CITY 2-0 LIGI KUU ENGLAND
 CHELSEA imejitanua kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Stoke City Uwanja wa Britania usiku.

The Blues ya kocha Mreno, Jose Mourinho sasa inatimiza pointi 42 baada ya mechi 17, ikiwazidi kwa pointi tatu, mabingwa watetezi, Manchester City waliocheza mechi 17 pia. Man United wenye pointi 32 ni wa tatu baada ya
kucheza mechi 17 pia.
John Terry aliifungia bao la kwanza Chelsea akimalizia mpira wa kona uliopigwa na kiungo Cesc Fabregas. Phil Bardsley alikuwa mwenye bahati kwa kuonyeshwa kadi ya njano tu baada
ya kumchezea rafu mbaya Eden Hazard.

Fabregas akaifungia bao la pili Chelsea zikiwa zimebakia dakika 12 kupulizwa kipyenga cha mwisho na kuwaweka sawa Th Blues kileleni.
Kikosi cha Stoke City kilikuwa; Begovic,
Bardsley, Shawcross, Muniesa, Pieters, Nzonzi, Cameron/Adam dk68, Walters, Bojan, Arnautovic/Assaidi dk82 na Crouch/Diouf dk63.


Chelsea; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry,
Azpilicueta, Mikel, Matic, Willian/Schurrle dk80, Fabregas, Hazard/Zouma dk90 na Costa/ Drogba dk85.


Comments