BEKI NEWCASTLE AJIGONGA KWENYE NGUZO NA KUCHANIKA JICHO


BEKI NEWCASTLE AJIGONGA KWENYE NGUZO NA KUCHANIKA JICHO
BEKI wa Newcastle, Steven Taylor amechanika karibu na jicho baada ya kujigonga kwenye nguzo ya lango kipindi cha pili jioni ya leo katika mchezo dhidi ya mahasimu, Sunderland
Uwanja wa St James' Park.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alifanikiwa kumzuia Steven Fletcher kuwafungia Sunderland wakati huo timu hizo zikiwa hazijafungana, lakini akachanika eneo la jichoni.

Taylor mara moja alipata huduma ya kwanza kutoka kwa timu ya madaktari wa Newcastle kabla ya kutolewa nje na kutibiwa kwa dakika saba kisha kurejea uwanjani na kushangiliwa kishujaa na mashabiki wa timu yake. Newcastle
ililala 1-0, bao pekee la Adan Johnson.
 Beki wa Newcastle, Steven Taylor akijigonga kwenye nguzo wakati wa kuokoa bao
 Taylor akipatiwa huduma ya kwanza na
madaktari wa Newcastle baada ya kuchanika eneo la jichoni




Comments