Shirikisho la soka dunia FIFA limeitupilia mbali rufaa iliyokatwa na klabu ya Barcelona kuhusu kuizuia kusajili kwa kukiuka kanuni ya usajili.
Barca walifungiwa kwa miezi 14 kusajili baada ya kufanya makosa kwa kusajili kinda wa chini ya miaka 18, Ikiwa ni kinyume na kanuni za usajili za Fifa.
Kwa maamuzi haya timu hii haitakua na uwezo wa kusajili mchezaji mpya mpaka Januari 2016.Barcelona wantarajia kukata rufaa tena maamuzi haya ya Fifa kwenye mahakama ya usuhuhishi michezoni(Cas).
Miamba hiyo ya soka ilifanikiwa kuwasajili mshambuliaji Luis Suarez , mabeki Thomas Vermaelen Jeremy Mathieu golikipa Claudio Bravo na kiungo Ivan Rakitic mwanzoni mwa msimu baada ya kupewa ruhusa maalumu na Fifa.
Tayari rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu, ameshutumu maamuzi hayo aliyodai yamekithiri upindishwaji mkubwa wa sharia.
Comments
Post a Comment