Mkufunzi          wa Liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa hana mipango ya          kumuuza mshambuliaji wa
        kilabu          hiyo Mario Baloteli wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi          Januari.
        Mshambuliaji          huyo mwenye umri wa miaka 24 na ambaye amefunga mabao mawili          katika mechi 15 amehusishwa na uhamisho wa Inter Milan kulingana          na gazeti dello Sport.
        ''Hicho          si kitu nilichofikiria kufanya,kusema ukweli'', alisema Rodgers.
        ''Tumekuwa          na mechi nyingi msimu huu na kwa sasa kitu muhimu ni kukiweka          kikosi hiki pamoja'',. Liverpool ilikuwa ya pili katika jedwali          la ligi ya Uingereza na walijulikana kwa mchezo wao wa
        kasi          na 'gusa' ni 'guse'.
        
Comments
Post a Comment