AZAM YAPOTEZA MECHI YAKE YA PILI KIRAFIKI UGANDA



AZAM YAPOTEZA MECHI YAKE YA PILI KIRAFIKI UGANDA

azama
Baada ya kupoteza mechi yake ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki katika kambi yake ya siku 10 nchini Uganda, Azam FC leo jioni imeoteza kwa bao 1-0 mechi yake ya pili dhidi ya URA ya nchini humo.

Azam FC, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), walipoteza mechi yao ya kwanza ya kirafiki nchini humo wakifungwa mabao 3-2 dhidi ya SC Villa ya Uganda na leo wamekubali kipigo hicho. Mechi zote zikichezwa jijini Kampala, Uganda.

Kikosi hicho cha Mcameroon Joseph Omog kitashuka tena uwanjani Jumamosi na Jumapili kumenyana na KCCA na Vipers FC, zote za Uganda kabla ya kurejea nchini Desemba 22 kusubiri mechi yao ya VPL dhidi ya Yanga itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Desemba 28.



Comments