Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Azam FC imesajili kipa mpya Khalid Mahadhi Ali kutoka Mafunzo FC ya Ligi Kuu ya Zanzibar.
Jaffar Idd Maganga ameuambia mtandao huku akiwa Kampala, Uganda mchana huu kuwa wamemsainisha mkataba wa miaka miwili kipa huyo kuwapa nguvu makipa wao.
"Tumesajili kipa mpya, usajili huo umefanyika ndani ya kipindi cha dirisha dogo. Kipa Mahadhi ataungana na timu itakaporejea Dar es Salaam Desemba 22 ikitokea hapa Kampala," amesema Maganga.
Mahadhi anaungana na Mzanzibar mwenzake kipa Mwadin Alli katika kikosi cha Mcameroon Joseph Omog cha Azam FC.
Comments
Post a Comment