AZAM FC WAREJEA NCHINI NA KUTIMKIA KAMBINI


AZAM FC WAREJEA NCHINI NA KUTIMKIA KAMBINI

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam

Baada ya kumaliza kambi yao ya siku 10 jijini Kampala, Uganda, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Azam FC wametua nchini kwa pipa na kuingia kambini moja kwa moja kujiandaa kwa mechi inayofuata dhidi ya Yanga SC.
azzz
Azam FC ilicheza mechi nne za kimataifa za kirafiki ikishinda moja tu (3-1 dhidi ya Vipers) na kupoteza tatu 3-2 dhidi ya SC Villa, 1-0 dhidi ya URA kabla ya 2-0 dhidi ya KCCA, itakuwa na kibarua kigumu mbele ya Yanga SC katika mechi ya raundi ya nane ya VPL msimu huu itakayochezwa Uwanja wa Taifa Jumapili.

Baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndehe wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini hapa leo saa 10 jioni, Saad Kawemba, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, amesema wamenufaika kwa mengi kutokana na kambi hiyo huku akikipelewka kambini tena jijini kikosi chake ili kiimarike zaidi kabla ya kuivaa Yanga.

Kikiwa Uganda, Kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Mcameroon Joseph Omog kilimsajili winga wa KCCA Brian Majwega na kumtema mshambuliaji Mhaiti Piere Saint-Preux.



Comments