Mfumo mama wa vilabu vingi duniani hususani vya soka uendeshwa kwa misingi ya wanachama na ndio wenye nguvu na ushawishi wa chochote ndani ya klabu zao.
Mfumo huu umekua ukibadilika kuendana na ukuaji wa sayansi na teknologia na hata baadhi ya wamiliki wapya wa vilabu wamekua wakiukwepa mfumo huo.
Nchini Tanzania vilabu vikongwe na pinzani vya Simba na Yanga ni moja wapo ya vilabu vinavyotumia mfumo wa wanachama ambao bado umekua hauvisaidii vilabu hivyo kupiga hatua kimaendeleo.
Wakati watu wakiviangalia vilabu hivyo kama mfano, hii leo klabu ya Azam fc inazindua kadi kwa ajili ya mashabiki wake kupitia bank ya NMB ambao kimsingi ndio wadhamini wa timu hiyo.
Maswali mengi yanayogonga vichwani mwa wachambuzi wa mambo ni je? Mfumo mpya wa kadi wa Azam fc utakua tofauti na ule wa vilabu vya Simba na Yanga?
Kikubwa ni kusubiri kuona Azam wanakujaje na mpango wao huo ambao kama utakuwa umeandaliwa vizuri unaweza kuisaidia timu hiyo kuongeza chanzo kingine cha mapato.
Comments
Post a Comment