ARSENAL YATENGA PAUNI MILIONI 20 KUMNASA WILLIAM CARVALHO WA SPORTING LISBON


ARSENAL YATENGA PAUNI MILIONI 20 KUMNASA WILLIAM CARVALHO WA SPORTING LISBON

William Carvalho (left) is a £20million target for              Arsenal in January 

Arsenal inajiandaa kurudi kwenye mawindo ya kumnyakua kiungo mkabaji William Carvalho (pichani kushoto) kutoka Sporting Lisbon ya Ureno katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Inaaminika kocha Arsene Wenger yuko tayari kuweka mezani kitita cha pauni milioni 20 kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 22.

Mazungumzo baina ya timu hizo mbili yalivunjika kiangazi kilichopita baada ya Sporting Lisbon kutaka malipo ya pauni milioni 30.

Lakini Arsene Wenger akiwa amekivusha kikosi chake kwenda hatua ya mtoano kwenye Champions League, anaamini ni wakati muafaka wa kuimarisha udhaifu wa safu yake ya ulinzi huku Carvalho akiwa ni mmoja wa wachezaji wachache wa kiwango cha juu watakaokuwa sokoni mwezi Januari. Hata hivyo hataweza kuitumikia Arsenal kwenye Champions League.

Sporting Lisbon ikiwa imetolewa kwenye Champions League, inaaminika itakuwa tayari kumuuza Carvalho.

 



Comments