LICHA ya kuwa pungufu baada ya Olivier Giroud kutolewa kwa kadi nyekundu, Arsenal imemudu kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya QPR katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku
huu Uwanja wa Emirates.
Katika mchezo huo, Alexis Sanchez alikosa penalti mapema kipindi cha kwanza baada ya mkwaju wake kuokolewa na kipa Rob Green, baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi
na Armand Traore.
Sanchez alisahihisha makosa yake dakika ya 37 baada ya kuifungia The Gunners bao la kwanza akimalizia krosi ya Kieran Gibbs, kabla ya Giroud kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja
kwa kwa kumpiga kichwa Nedum Onuoha.
Tomas Rosicky akaifungia bao la pili Arsenal dakika ya 65 akimalizia pasi nzuri ya Sanchez, kabla ya Charlie Austin kuifungia bao la kufutuia machozi QPR kwa penalti dakika ya 79.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny;
Debuchy, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Flamini , Sanchez, Rosicky/Chambers dk83, Cazorla, Welbeck/Coquelin dk87 na Giroud.
QPR; Green, Isla, Onuoha, Ferdinand, Caulker, Traore/Hoilett dk62, Mutch/Zamora dk72, Henry/Fer dk62, Kranjcar, Vargas na Austin.
Comments
Post a Comment