Kiungo wa West Ham Alex Song amefichua kuwa matarajio yake ilikuwa ni kurejea Arsenal baada ya kuondoka Barcelona kiangazi kilichopita, lakini Arsene Wenger hakumtaka.
Song ambaye amekuwa kwenye kiwango bora tangu aliporejea England, alichagua kujiunga na West Ham wakati Arsenal ikigoma ikigoma kuimarisha safu yake ya kiungo.
Nyota huyo wa Cameroon, amedai yaliyomkuta ni yale yale yaliyomkumba Cesc Fabregas ambaye alitaka kurejea Arsenal lakini akaangukia Chelsea.
Comments
Post a Comment