Real Madrid imetibua rekodi yake ya kutofungwa tangu mwezi Septemba baada ya kukubali kipigo cha 4-2 kutoka kwa AC Milan katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Dubai Jumanne jioni.
Stephan El Shaarawy alifunga mara mbili katika dakika ya 31 na 49 huku Menez akifunga dakika ya 24 na Pazzini akimalizia kwa bao la dakika ya 73.
Ronaldo aliifungia Real Madrid bao muhimu dakika ya 35 likiwa ni la kusawazisha kabla ya AC Milan haijacharuka na kuangusha karamu ya magoli huku Karim Benzema akiipunguzia aibu timu yake kwa kufunga bao la pili kwa njia ya penalti dakika ya 84.
Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti aliingia mapumziko ya majira ya barafu akiwa na rekodi ya kushinda mechi 22 mfululizo lakini makamanda wake Cristiano Ronaldo na wenzake wakafichwa na AC Milan inayosota nafasi ya saba kwenye msimamo wa Serie A.
Kwa ushindi huo, AC Milan wakatwaa kombe maalum la Dubai Football Challenge.
Comments
Post a Comment