ZLATAN ATUPIA KWA PENATI PSG IKISHINDA 1-0 DHIDI YA NICE.


Zlatan Ibrahimovic ameendelea kung'ara baada ya kuifungia PSG bao pekee ilipoilaza Nice 1-0.
Katika mechi hiyo iliyokuwa ngumu, Zlatan alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 15 baada ya kiungo Mbrazili, Lucas Moura kufanyiwa madhambi.
Kutokana na ushindi huo, PSG imejiimarisha katika nafasi ya oili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Ufaransa, huku ikiwa inazidiwa pointo moja tu na vinara Marseille.

Comments