YANGA WAPANIA KULIPA KISASI AZAM KWA KUMCHUKUA KIPA MWADINI ALI


YANGA WAPANIA KULIPA KISASI AZAM KWA KUMCHUKUA KIPA MWADINI ALI

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Baada ya matajiri wa Dar es Salaam, Azam FC kuwanasa nyota wawili kutoka Yanga, kiungo mzawa Frank Domayo na mshambuliaji Didier Kavumbagu raia wa Burundi, uongozi wa wanajangwani unaonekana kupania kulipa kisasi kwa kunasa saini ya kipa Mwadin Ali kutoka kwa wanalambalamba.
Mtandao wa goal.com umeripoti muda mfupi uliopita kwamba Yanga SC ipo mbioni kumsajili kipa huyo chaguo la kwanza kwenye kikosi cha kocha Mcameroon Joseph Omog cha Azam FC kwa dau la Sh. milioni 60 katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.
Imeelezwa kuwa viongozi wa kamati ya usajili ya klabu ya Yanga bado wapo katika mazungumzo na kipa huyo wakimshawishi kujiunga na mabingwa hao mara 24 wa Tanzania Bara ili kuziba nafasi ya Juma Kaseja anayesemekana kutaka kujiunga na timu yake ya zamani, Simba.
mwa
Mwadini ameongea na mtandao huo na kukiri kuzungumza na viongozi wa Yanga na kusema endapo ataridhika na maslahi, atakuwa tayari kujiunga na timu hiyo yenye upinzani mkubwa na timu yake ya sasa Azam FC.
Yanga SC wana kipa chaguo la kwanza Taifa Stars kwa sasa Deogratius Munishi 'Dida' ambaye walimchukua pia kutoka Azam FC.
Mkataba wa Mwadini unamalizika Oktoba 2015 na kipa huyo amesema miaka minne aliyoichezea timu hiyo akitokea Mafunzo ya Zanzibar inatosha na anataka kusaka changamoto mpya.



Comments