“WENGER ANATAKIWA KUKIRI MAKOSA NA KUIMARISHA NAFASI ZOTE, ILI TUSHINDANE NA CHELSEA NA MAN CITY”:USMANOV
Mmiliki ambae ana hisa nyingi wa pili wa klabu ya Arsenal          Alisher Usmanov, amemtaka Wenger akiri makosa yanayosababisha          matokeo mabaya ya timu hiyo, pamoja na kwamba anamsapoti kwa          kiwango kikubwa menaja huyo…
          
Alisher Usmanov ana shea nyingi kwenye klabu hiyo akiwa nyuma ya Stan Kraonke, anasisitiza kwamba zinahitajika fedha nyingi kuifanya Arsenal iingie kwenye ushindani mkubwa..
Anasema kwamba, kama unakuwa hukubali makosa hata kama uko juu, na wewe ni Genius si rahisi kurudia kwenye level yako…lakini ukikubali basi utarejea kwenye level yako ya juu uliyozoeleka mwaka hadi mwaka..
Bado anaheshima kubwa kwa raisi wa klabu, lakini pia Wenger kwake si kocha wa Ulaya bali ni kocha wa level ya kidunia…kwenye football..
Kama kuna vitu ambavyo Usmanov hakutaka kuviweka wazi, ni suala la kusajili mchezaji wa kiwango cha juu wa kiungo cha ulinzi, akisema hiyo ni kazi ya kocha, na haa uwezo wa kumfundisha cha kufanya,ila kwake muhimu ni kuona kwamba, kila nafasi inaboreshwa ndani ya kikosi…
          Muhimu kwake ni kuona kuwa klabu inakuwa na ushindani wa kweli          ndani na nje ya England na kuwa na ushindani na klabu kama          Chelsea , Manchester City, Real, Barcelona, Paris Saint-Germain,          Bayern na nyingine.
La mwisho akasisitiza kwamba, hajawahi kuzungumzia biashara ya kuuza hisa zake kwa mwenzake Stan Kraonke, ama yeye kununua hisa za mwenzake…
Usmanov aliyewahi kuwekwa ndani na serikali ya bwana Mikhail          Gorbachev si chini ya miaka 6, kwa makosa ya jinai ,kabla ya          kutolewa amekuwa na wakati mgumu mno kwa wapenzi wa soka wa          klabu hiyo ya London… pamoja na kwamba ni bilionea, lakini wapo          wapenzi wa Arsenal wanaomuona kuwa hana mapenzi na klabu hiyo na          hawamtaki, kiasi cha kumbebea mabango kwenye mechi zao kwamba          wanamchukia…
          
          Kukosa taji la Premier tangia msimu wa 2003/04,,,….Wenger          amefeli ama klabu imefeli???????
Comments
Post a Comment