Wakati RVP akiwa kwenye kiwango kibovu – Falcao arudi dimbani



Wakati RVP akiwa kwenye kiwango kibovu – Falcao arudi dimbani

236F455300000578-2846451-image-1_1416770488444Baada ya kuandamwa na majeruhi yaliyomuweka nje ya uwanja kwa mechi takribani nne hatimaye jana jumapili Radamel Falcao amezima tetesi za juu ya majeruhi yake baada ya kurudi uwanjani na kufanya mazoezi yote na wachezaji wenzie – na sasa anategemewa kurudi dimbani katika mechi dhidi ya Hull City wikiendi ijayo.
Mshambuliaji huyo wa Colombia amekuwa akisumbuliwa na jeraha la misuli nyuma ya mguu, alijiunga na United siku ya mwisho ya usajili lakini mpaka sasa hajawahi kucheza mechi na kumaliza dakika 90 akiwa na jezi ya United.

Lakini sasa amerudi dimbani na amemhakikishia kocha Louis Van Gaal kwamba yupo tayari kuisadia timu yake katika mapambano ya EPL.
Habari imekuwa nzuri kwa kocha LVG ambaye amekuwa akiiona timu yake ikipata taabu katika kuzifumania nyavu za timu pinzani, pamoja na ushindi waliopata jumamosi dhidi ya Arsenal.
Fomu ya Robin van Persie kila siku inazidi kuwa ya kusikitisha, na United wamekoa huduma nzuri katika safu ya ushambuliaji.
Falcao amaefunga mara moja katika klabu yake mpya – dhidi ya Everton, jana alitweet kwa kuandika:

236F23E500000578-0-image-25_1416768721883
Swali lilobakia ni je Van Gaal atamsaini Falcao kwa uhamisho wa kudumu mwisho mwa msimu au hali itakuwa tofauti?



Comments