Jean de Dieu Makiese alizaliwa May 28, 1952 katika jiji la Kinshasa huko Kongo, jina alilokuja kujulikana sana ni Madilu System, alikuwa mtunzi na muimbaji mzuri sana aliyeanza mambo ya muziki 1969 akiwa na Orchestre Symba, baadae Orchestre Bambula iliyokuwa ikiongozwa na Papa Noel, baadae akajiunga na Festival des Maquisards iliyokuwa ikiongozwa na Sam Mangwana baadae Madilu alianzisha bendi yake iliyoitwa Orchestre Bakuba Mayopi.
Lakini alipojiunga na TP OK Jazz ya Franco ndipo alipokuja kupata umaarufu wa kimataifa. Franco ndie aliyempa jina la Madilu System. Tungo yake ya kwanza na TP OK Jazz ilikuwa Mamou (Tu Vois),wimbo uliotamba sana 1984, akafuatia na kibao cha Pesa Position kisha Mario na Reponse de Mario 1985, mwaka 1989 aliangusha kile kigongo cha La Vie des Hommes. Madilu System, The Ninja alifariki August 11, 2007. Tumwone hapa akiwa jukwaani 'live' na Pesa Position
Comments
Post a Comment