TOURE: RODGERS HANA TOFAUTI NA ARSENE WENGER


TOURE: RODGERS HANA TOFAUTI NA ARSENE WENGER

ROY
Mlinzi wa kati wa klabu ya Liverpool, ndugu wa kiungo Yaya Toure, Kolo Toure amesema kuwa meneja wa majogoo hao wa Anfield Brendan Rodgers anamkumbusha enzi za kocha wake wa zamani Arsene Wenger na hivyo anaamini ataubadili msimu mbaya klabuni hapo.
Ikumbukwe kuwa, klabu hiyo la liverpool imekuwa na mwenendo mbaya siku za karibuni kufuatia kupoteza mechi nne mfululizo kabla ya kuambulia sare kunako michuano ya klabu bingwa ulaya dhidi ya Ludogorets ya Bulgaria jumatano usiku.
Liverpool inashika nafasi ya 12 katika ligi ya uingereza pamoja na kuwa miongoni mwa timu zilizofanya vizuri msimu ulopita, lakini Kolo Toure bado anaamini ndiye meneja sahihi anayepaswa kuendelea kuinoa miamba hiyo na kuikwamua pale ilipo. Nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji walounda kikosi cha Arsenal kilichomaliza msimu bila kupoteza 2003-04
Mchezaji huyo pia alipata kushinda taji la ligi kuu ya uingereza msimu wa 2012 akiwa na klabu cha Manchester City lakini bado anaamini meneja wake huyo wa Liverpool, Brendan Rodgers anashabihiana na Arsene wenger. "namwona wenger ndani yake kwani ana akili" alieleza Liverpool Echo:
"Anajua namna ya kuongea na wachezaji, na namna ya kuwatumia ipasavyo, nina uhakika atalithibitisha hilo mara atapoikwamua klabu katika kipindi hiki kigumu" "kama Arsene daima amekuwepo mazoezini ili kuboresha mambo, hata mbinu zao zinafanana kwani daima amekuwa akituhimiza kucheza soka la pasi na kumiliki"
ROY 1
Toure (33) ameendelea kusisitiza kuwa klabu ya Liverpool inapaswa kuendela kumuunga mkono Rodgers, wakatio akiendela kuboresha mambo kunako michuano ya klabu bingwa ulaya. "tunapaswa kuendelea naye maana yeye ni mmoja wa makocha bora katika ligi ya uingereza".
"siku zote kama meneja wa timu unahitaji muda, ni kama msimu uliopita ulivyokuwa wa kushangaza pamoja na kwamba mambo ni magumu kwa sasa ila bado naamini amefanya kazi kubwa na hivyo kama timu tunampenda, michuano ya ulaya ni migumu ndo sababu ukitizama hata vilabu kama Manchester City unapata funzo".
"Daima amekuwa akijitoa kwa kila kitu, tizama namna alivyofanya mambo makubwa katika kipindi kifupi. Alipokuja hapa hali ilikua mbaya lakini alibadilisha kila kiyu, naamini hata safari hii itafanikiwa. Alimalizia nyota huyo.



Comments