Pascal-Emmanuel Sinamoyi Tabu alizaliwa Bagata, Congo. Umaarufu wake katika muziki ulianzia mwaka 1956 alipoimba jukwaa moja na Joseph "Le Grand Kallé" Kabasele, na bendi yake ya L'African Jazz. Alijiunga kamili na bendi hii baada ya kumaliza shule, na alikuwa muimbaji moja wapo wa wimbo Independence Cha Cha ambao Joseph Kalle aliutunga kwa ajili ya uhuru wa Kongo toka kwa Wabelgiji mwaka 1960. Tabu Ley alikaa na African Jazz mpaka mwaka 1963 ambapo yeye na Dr. Nico Kasanda walipoanzisha kundi lao la African Fiesta ambalo wengi hulitambua kama ndilo kundi lililoanzisha muziki mpya wa soukus ya Kongo.
Nicolas Kasanda wa Mikalay alizaliwa July 7, 1939 na kufariki September 22, 1985) alijulikana zaidi kama Docteur Nico, alizaliwa katika jimbo la Kasai huko Kongo, alianza muziki akiwa na miaka 14 katika kundi la African Jazz, Alikuwa mpigaji mkali sana kiasi cha kwamba wakati mmoja alipozuru Paris Jimi Hendrix mmoja ya wapiga magitaa walioheshimika sana duniani alimtembelea kwenda kumsikiliza. Alianzisha stail yake ya upigaji wa gitaa la solo na walipoanzisha bendi ya African Fiesta na Tabu Ley walitambulika na kuheshimika Afrika nzima mpaka leo hii
Comments
Post a Comment