ZURICH,L Uswisi
KAMA ilivyotarajiwa, matokeo ya sare ya bao moja dhidi ya timu kibonde ya taifa ya Swaziland, yameiponza Tanzania baada ya kushuka kwenye viwango vya kila mwezi vilivyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) leo.
Tanzania imeshuka kwa nafasi mbili kutoka 110 duniani mwezi uliopita hadi 112 mwezi huu ikiwa nafasi ya 32 barani Afrika huku Swaziland ikipanda kwa nafasi mbili hadi 162 duniani.
10 bora ya dunia inaendelea kuongozwa na mabingwa wa Kombe la Dunia, Ujerumani wakifuatwa na Argentina, Colombia, Ubelgiji, Uholanzi, Brazil, Ureno, Ufaransa, Hispania na Uruguay walioshuka kwa nafasi mbili.
Algeria licha ya kushuka kwa nafasi tatu, bado wanaendelea kuongoza barani Afrika wakiwa nafasi ya 18 duniani wakifuatwa na Tunisia (22 duniani), Ivory Coast (24), Senegal (35), Ghana (37), Guinea (38), Cape Verde (39), Cameroon (41), Nigeria (42) na Mali (49) wanaokamilisha 10 bora barani.
Afrika Mashariki inaongozwa na Uganda waliopanda kwa nafasi sita wakiwa nafasi ya 20 barani Afrika na 78 duniani wakifuatwa na Rwanda (24, 90), Tanzania, Kenya (33,114) na Burundi (40, 124).
Uganda pia inaongoza Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ikifuatwa na Rwanda, Ethiopia (31, 110), Tanzania, Kenya, Sudan (34, 115), Burundi, Shelisheli (50, 174), Sudan Kusin (51, 189)i, Mauritius (52, 191), Eritrea (53, 202), Djibouti (54, 204) na Somalia walioko nafasi ya mwisho barani Afrika na duniani (55, 206).
Comments
Post a Comment