STAND YATUA JANGWANI KUWASAJILI BAHANUNZI, THABIT



STAND YATUA JANGWANI KUWASAJILI BAHANUNZI, THABIT

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
UONGOZI wa Stand United inmayoshiririki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu, umesafiri kutoka usukumani mjini Shinyanga hadi maeneo ya Jangwani jijini hapa kuzungumza na uongozi wa Yanga SC ili uwasajili Said Bahanunzi, Omega Seme na Hamis Thabit kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Stand United, Muhibu Kanu ameuambia mtandao huu jijini hapa leo kuwa ameamua kuja kuteta na uongozi wa Yanga SC ili aruhusiwe kuwanasa wachezaji hao kuimarisha kikosi chao kilichop[o nfasi ya 10 katika msimamo wa VPL kikiwa na pointi tisa sawa na Mgambo walioko nafasi ya tisa, Polisi Morogoro (8) na Simba (7).

stand
Mashabiki wa Stand United wakiingia kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga kabla ya kuanza kwa mechi ya timu yao iliyopita dhidi ya Yanga. Stand ililala 3-0
"Kuna baadhi ya wachezaji wetu tutakosa huduma zao kwa sababu wanatakiwa na timu za ndani na nje ya nchi. Musa Said anatakiwa na Kaizer Chief ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Heri Halifu anatakiwa na Mbeya City," kiongozi huyo amesema.
"Kuna wengine wanatakiwa na JKT Ruvu, hivyo tunaona tuje Yanga kusaka wachezaji watakaotuongezea nguvu. Tayari tumezungumza na uongozi wa Yanga, wametuambia tuandike barua na tumefanya hivyo maana pesa ipo."
Aidha, Mkurugenzi huyo amesema wanamnyatia pia mchezaji Jamil Mchaulu 'Balotelli' wa Azam FC na kwamba tayari wameshaundikia barua uongozi wa wanalambalamba juu ya suala hilo.
Amesema wachezaji wote hao wanawataka kwa mkopo.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu na Meneja wa Timu ya Azam, Jemedari Said wamekiri kupokea maombi ya Stand United.
"Masuala yote ya wachezaji yako chini ya kocha mkuu (Marcio) Maximo. Atakapowasili nchini Jumatano tutamweleza, kama ataona inafaa kuwaachia wachezaji hao tutaruhusu," amesema Njovu.
Bahanunzi, aliyeibuka mfungaji bora wa Kombe la Kagame mwaka juzi katika msimu wake wa kwanza Yanga SC akitokea Azam FC, amekuwa akisugua benchi katika kikosi hicho cha Jangwani, hivyo kuonekana kama hana lolote.



Comments