Klabu bingwa ya zamani nchini, Simba SC iko katika harakati za kuhakikisha wanamsaini mlinzi mahiri wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu na vinara hao wa ligi kuu Tanzania Bara. Mbonde ameonyesha uwezo mkubwa katika safu ya kati ya ulinzi kikosini Mtibwa alikuwa ajiunge na Simba wakati wa usajili wa katikati ta mwaka lakini mchezaji huyo alikataa baada ya Simba kutaka kumsajili kwa njia zisizo halali.
Chipukizi huyo ambaye amepata sifa kubwa kutkana na kuwathibiti washambu;iaji ka Geilson Santos Jaja al;iyekuwa Yanga SC na Amis Tambwe wa Simba alitakiwa na Simba lakini aligoma.
" Ni kweli Simba wamekuwa wakinihitaji kwa muda mrefu" anasema mlinzi huyo, " Nilikataa kwa sababu walinilazimisha mimi ndiye nivunje mkataba na timu yangu wakati taratibu haziko hivyo, naweza kucheza timu yoyote kama taratibu za uhamisho wangu zitakamilika kwa taratibu"
Simba inasaka mlinzi wa kati ambaye ataungana na nahodha, Joseph Owino, Hassan Isihaka na Joram Mvegeke. Kocha mkuu wa timu hiyo Patrick Phiri anamuhusudu mlinzi huyo wa Mtibwa .
Comments
Post a Comment