SIMBA HATUJASAJILI MCHEZAJI DIRISHA DOGO



SIMBA HATUJASAJILI MCHEZAJI DIRISHA DOGO

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
LICHA ya uvumi kwamba Simba imefanikiwa kumnasa mshambuliaji wa Gor Mahia na timu ya taifa ya Uganda, Dan Sserunkuma, uongozi wa klabu hiyo umeweka wazi kwamba mpaka sasa bado haujasajili mchezaji hata mmoja katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.
Msemaji wa Simba, Hamphrey Nyasio amesema Dar es Salaam leo kuwa klabu hiyo bado haijafanikiwa kunasa saini ya mchezaji hata mmoja hadi sasa.
Lakini, mtandao huu unatambua kwamba licha ya kupewa ofa nono na klabu yake ya sasa Gor Mahia ili aendelee kubaki katika Ligi Kuu ya Kenya (KPL), Sserunkuma ametua jijini Dar es Salaam leo mchana kufanya mazungumzo na uongozi wa Simba kwa lengo la kusajiliwa.
dan
Hata hivyo, uongozi wa juu ya klabu hiyo hautaki kuweka suala hilo hadharini hadi pale mambo yatakapokuwa yamekamilika.
"Kocha mkuu (Mzambia Patrick Phiri) anatarajia kuwasili nchini leo (jana) jioni, (Amissi) Tambwe na (Pierre) Kwizera waliwasili juzi (Jumanne) jioni na wanaendelea vizuri na mazoezi. Hakuna mchezaji mpya ambaye mpaka sasa Simba imefanikiwa kumsajili," Nyasio amesema.
"(Emmanuel) Okwi na (Joseph) Owino wa=natarajiwa kuwasili nchini kesho," amesema Nyasio.
Kumekuwa na taarifa zinazodai kwamba Sserunkuma, mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL), ameshamalizana na Simba huku klabu yake ya sasa Gor Mahia ikitangaza jana kupitia kwa Katibu Mkuu, Chris Omondi kwamba iko katika hatua za mwisho kumwongeza muda wa kuendelea kubaki kwa mabingwa hao wa Kenya.
Kama Simba watashindwa kumalizana naye jijini Dar es Salaam kwa sasa, ni wazi kuwa nyota huyo wa Cranes atarejea Kenya kuongeza muda wa kuendelea kukipiga na Gor Mahia.



Comments