Sikia hiki kisa cha wanandinga wetu wa kiafrika…AMBAO KILA KUKICHA HAWAISHI VITUKO…


Sikia hiki kisa cha wanandinga wetu wa kiafrika…AMBAO KILA KUKICHA HAWAISHI VITUKO…

Hiki kinamuhusu winga wa kimataifa wa Ivory Coast anaekipiga klabu ya AS Roma ya Italia Gervinho.

ger

Kijana baada ya mechi ya kuwania kufuzu kwa fainali za kandanda za kombe la mataifa ya bara la Afrika dhidi ya Cameroon juma lililopita, alitakiwa kurejea mapema nchini Italia….

AS Roma wakamtumia Gervinho ndege binafsi ya kumfanya awahi kurejea kwenye majukumu ya klabu yake nchini Italia, lakini kijana akawa na mzigo wa ziada, na huu usifikiri ni begi, bali alichukuwa mlimbwende huyooo unaeomuona hapo..

Ndege iliyokodiwa ilikuwa na nafasi moja tu ya Gervinvo, sasa kijana huyu ili kupita vikwazo hapo Airport akalazimika kuhonga maofisa wanne uwanjani hapo, akapita na kisha akaenda kwa Rubani, hapo mambo ndio yakawa magumu kwani alikataa…

Baada ya kukataa ikabidi mdada abakie, lakini nyuma mambo yakawa mabaya kwa wale maofisa waliohongwa na sasa wametimuliwa kazi, baada ya tukio hilo,,,,

Huu ndio UAFRIKA WETU!!!!!!…KIPAJI PEKEE HAKITOSHI KWA MAISHA YA STAA YOYOTE..



Comments