REAL MADRID YAWEKA REKODI MPYA KWA KUSHINDA MICHEZO 16 MFULULIZO



REAL MADRID YAWEKA REKODI MPYA KWA KUSHINDA MICHEZO 16 MFULULIZO

Gareth Bale, Carlo Ancelotti na Sergio Ramos wakiwa wameshikilia vidole 16 kushangilia wimbi la ushindi la Real Madrid WINGA Gareth Bale, beki Sergio Ramos na kocha wao, Carlo Ancelotti wakisherehekea kushinda mechi 16 mfululizo kwa mara ya kwanza katika historia ya Real Madrid.
Watatu hao waliweka picha kwenye mtandao wa Twitter jana usiku bada ya kuifunga Malaga 2-1, mabao ya Karim Benzema na Bale na kuweka rekodi hiyo, wakishikilia vidole 16 baina yao na Ramos akasema: 'A seguir trabajando. Buenas noches..!! maana yake Acha tuendelee kupiga kazi. Usiku mwema..!!.'
Ushindi huo wa La Liga unaifanya klabu hiyo ipiku rekodi ya mechi 15 iliyowekwa na Miguel Munoz msimu wa 1960-61 na kufikiwa pia na Jose Mourinho msimu wa 2011-12.
Bale (kushoto) akishangilia na Karim Benzema usiku wa jana baada ya kuichapa 2-1 Malaga
WIMBI LA USHINDI REAL MADRID MECHI 16
1. Real Madrid 5-1 Basel (Ligi ya Mabingwa) - Septemba 16
2. Deportivo la Coruna 2-8 Real (La Liga) - Septemba 20
3. Real 5-1 Elche (La Liga) - Septemba 23
4. Villarreal 0-2 Real (La Liga) - Septemba 27
5. Ludogorets 1-2 Real (Ligi ya Mabingwa) - Oktoba 1
6. Real 5-0 Athletic Bilbao (La Liga) - Oktoba 5
7. Levante 0-5 Real (La Liga) - Oktoba 18
8. Liverpool 0-3 Real (Ligi ya Mabingwa) - Oktoba 22
9. Real 3-1 Barcelona (La Liga) - Oktoba 25
10.UD Cornella 1-4 Real (Kombe la Mfalme) - Oktoba 29
11.Granada 0-4 Real (La Liga) - Novemba 1
12. Real 1-0 Liverpool (Ligi ya Mabingwa) - Novemba 4
13. Real 5-1 Rayo Vallecano (La Liga) - Novemba 8
14. Eibar 0-4 Real (La Liga) - Novemba 22
15. Basel 0-1 Real (Ligi ya Mabingwa) - Novemba 26
16. Malaga 1-2 Real (La Liga) - Novemba 29


Comments