Watanzania wanatakiwa                kupigia kura jezi ya timu ya Taifa ya nyumbani na ugenini                kupitia mtandao wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania                (TFF) wa www.tff.or.tz ambapo jezi hizo                zimewekwa.
        TFF ilipokea mapendekezo                ya mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa kutoka kwa                Watanzania 86. Jezi 11 za nyumbani, bukta nane za                nyumbani, jezi nane za ugenini na bukta tano za ugenini                ndizo zimepitishwa kwa ajili ya kupigiwa kura.
        Mwisho wa kupiga kura ni                Desemba 31 mwaka huu. Mpigaji kura anatakiwa kubonyeza                kwenye jezi na bukta ambayo ameichagua. Anatakiwa kufanya                hivyo kwa jezi ya nyumbani na jezi ya ugenini.
        Tunawashukuru wote                waliojitokeza kupendekeza mwonekano mpya wa jezi ya timu                ya Taifa.
        IMETOLEWA NA SHIRIKISHO                LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
                

Comments
Post a Comment