Kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakiripotiwa kuwa ndoa yao ipo kwenye mawe lakini kwa picha zilizotoka hivi karibuni inaonyesha kwamba nahodha wa zamani wa Rwanda – Amavubi Hamad Ndikumana na mkewe muigizaji Irene Uwoya bado wana mahaba moto moto.
Irene na Ndikumana walioana miaka 5 iliyopita jijini Dar es Salaam, juzi walipigwa picha wakiwa uwanja wa ndege nchini Rwanda ambapo Irene alikuwa akiondoka nchini humo kurudi Tanzania anapoishi.
Ndikumana kwa sasa anayeichezea klabu ya Espoir ya Rwanda, hivyo yeye na mkewe wanaishi tofauti.
Comments
Post a Comment