Mesut Ozil; ‘Kushinda mataji ndiyo kila kitu kwa mchezaji’


info_1405708405Kiungo wa timu ya Taifa ya Ujerumani na klabu ya Arsenal, Mesut Ozil amesema kuwa atakuwa mchezaji bora zaidi chini ya mwalimu Arsene Wenger katika kikosi cha Arsenal. Mchezaji huyo aliye majeruhi kwa sasa anaendelea vizuri kutokana na majeraha yake ya goti ambayo aliyapata mwezi uliopita.

 

Ozil atarejea uwanjani baadae mwakani; " Wenger anajua kwamba natakiwa kupona haraka ili nirudi uwanjani, ananiamini sana, name najua kuwa yeye ni muhimu, namwamini sana. Kwa timu nzima kila mmoja anajua kwamba tunahitaji kupata mataji. Kwetu sisi wachezaji, mataji ndiyo kila kitu. Tunatakiwa kupambana kupata mataji. Binafsi najivunia kuwa hapa"

 

Ozil, 26 ambaye alishinda ubingwa wa kombe la dunia akiwa na kikosi cha UJerumani amekuwa akicheza kwa kiwango cha chini katika klabu ya Arsenal ambayo ilimsaini mwaka uliopita kutoka Real Madrid ya Hispania kwa ada ya rekodi ya klabu, euro 42 milioni ameongeza kwa kusema kuwa tangu akiwa na miaka 16 amekuwa akijua kuwa maisha yake ni mpira w miguu.

 

" Wala sijali yanayosemwa na vyombo vya habari kuhusu maisha yangu ya soka. Ninachofanya ni kutazama nini kinakuja mbele yangu" . Arsenal itacheza na Manchester United mwishoni mwa wiki hii katika ligi kuu ya England, Ozil hatakuwepo katika mchezo huo.

 

 



Comments