MESSI AWEKA REKODI NYINGINE, HAKUNA KAMA YEYE CHAMPIONS LEAGUE … Suarez naye aanza kufanya vitu vyake
Barcelona imeifumua APOEL Nicosia 4-0 katika mchezo wa upande mmoja wa Champions League huku mshambuliaji wake nyota Lionel Messi akifunga magoli matatu na kuweka rekodi mpya Ligi ya Mabingwa.
Kwa magoli hayo, Messi anakuwa ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi katika historia ya Ligi ya Mabingwa akiwa ametikisa nyavu mara 74 akimzidi kwa magoli mawili mkongwe wa Real Madrid Raul huku mpinzani wake mkubwa Cristiano Ronaldo mwenye magoli 70 akishika nafasi ya tatu.
Messi alifunga katika dakika ya 38, 58 na 87 huku mshambuliaji mpya Luis Suarez akifunga bao lake la kwanza kwa Barcelona kunako dakika ya 27.
Wikiendi iliyopita, Messi aliweka rekodi nyingine ya kuwa mfungaji mwenye magoli mengi La Liga akivunja rekodi ya tangu mwaka 1955.
Comments
Post a Comment