Messi aweka historia mpya La Liga, C. Ronaldo akifunga mara mbili……..



Messi aweka historia mpya La Liga, C. Ronaldo akifunga mara mbili……..

Mshindi mara nne wa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia, Leonel Messi alifunga ' hat-trick' yake ya kwanza msimu huku akiweka rekodi ya ufungaji wa mabao katika ligi ya La Liga. Mshambulizi huyo Muargentina mwenye miaka 27 aliisaidia klabu yake ya FC Barcelona kuivurumisha Seville kwa mabao 5-1 katika uwanja wa Camp Nou.

Messi amekuwa mfungaji bora wa muda wote katika historia ya ufungaji katika ligi ya La Liga. Messi amefikisha jumla ya mabao 253, mabao mawili zaidi ya Termo Zarra ambaye alifunga mabao 151 katika misimu 15 akiwa na klabu za Bilbao na Real Madrid.

Mshambuaji wa Brazil, Neymar Jr alifunga bao lake la 11 katika michezo 11 ya msimu huu dakika mbili baada ya mlinzi, Jordi Alba kujifunga na kuisawazishia Sevilla. Mchezaji wa zamani wa Sevilla, Ivan Rakitik alifunga bao la tatu katika dakika ya 65, kabla ya Messi kufunga tena katika dakika za 72 na 78. Kwa matokeo hayo, Barca imesogea hadi katika nafasi ya pili wakiwa nyuma ya vinara Real Madrid kwa tofauti ya pointi mbili.

Real iliishinda Elber kwa mabao 4-0 katika uwanja wa Estadio Municipal de Ipurua. Mwanaska bora wa dunia, Cristiano Ronaldo alifunga mara mbili na kufikisha mabao 20 katika michezo 11 msimu huu. Kiungo-mshambulizi James Rodriguez alifungua akaunti ya mabao baada ya kufunga bao lake la tano msimu huu katika dakika ya 23 kabla ya Ronaldo kufunga la pili dakika 20 baadae. Karim Benzema alifunga bao lake la saba msimu huu na kuifanya Real kuwa mbele kwa mabao 3-0 katika dakika ya 69.

C.Ronaldo alifunga kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 83 na kufikisha bao la 25 kwa michuano yote msimu huu. Kocha wa Real, Carlo Anceltti aliwapanga mastaa wake, Isco, Ton Kroos, Rodriguez, Garreth Bale, Ronaldo na Benzema katika kikosi cha kwanza.

Wakicheza katika uwanja wa nyumbani Vicente Calderon, mabingwa watetezi, Atletico Madrid walichomoza na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Malaga na kujivuta hadi katika nafasi ya nne. Atletico wapo nyuma ya vinara Real Madrid kwa tofauti ya pointi nne. Kiungo, Thiago Mendes alifunga bao la kyuongoza kwa timu yake katika dakika ya 12, kisha mshambulizi Mfaransa, Antoine Griezmann akaongeza lingine na kuwafanya vijana wa Mwalimu, Diego Simeone kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0.

Mshambulizi wa zamani wa Bayern Munich, Blackburn na Manchester City, Roque Santa Cruz alifunga bao la kufutia machozi kwa wageni kabla ya mlinzi Diego Godin kufunga bao la tatu kwa timu yake. Katika mchezo wa mwisho siku ya jana, Derpotivo la Coruna ililazimishwa suluhu-tasa na Real Sociedad katika uwanja wa Riazor/ Ligi hiyo itaendelea Jumapili hii kwa michezo minne. Rayo Valcano watacheza na Celta Vigo. Levante watawakaribisha Valencia, Elche wakicheza dhidi ya Cordoba na mchezo wa mwisho ni ule wa Villareal dhidi ya Getafe.

IMG_8987.JPG



Comments